Uza kwa simu ya Android, skani barcode kwa kamera yake, na uone mauzo, stock, matumizi na madeni ya wateja popote ulipo. Unaipakua Google Play, unaingia kwa namba yako ya simu, na duka lile lile linafunguka kwenye kompyuta pia.
Chagua bidhaa au skani barcode kwa kamera, pokea cash, M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money au HaloPesa, na muuzo umerekodiwa.
Kila muuzo, matumizi na malipo yanaingia kwenye kumbukumbu za biashara papo hapo. Hakuna daftari la kujaza usiku.
Ona kilichobaki, kinachokaribia kuisha na kilichoingia leo, bila kufika dukani.
Ona nani anadaiwa, kiasi gani na tangu lini, na urekodi malipo anapolipa. Kwenye kifurushi cha Mwanzo na kuendelea.
Mteja anapata risiti yake kwenye WhatsApp anapolipa, au unaichapisha kwenye printa ya risiti.
Kila mfanyakazi anaingia kwa msimbo wa duka na PIN yake, kwa hiyo kila muuzo una jina la aliyeuza.
Muuzo uliofanywa bila mtandao unahifadhiwa kwenye simu na kutumwa mtandao ukirudi. Unaona kinachosubiri.
App ya mauzo ni programu ya simu inayorekodi kila muuzo unapofanyika na kutunza kumbukumbu za biashara — mauzo, stock, matumizi na madeni — mahali pamoja. Badala ya daftari na kalamu, unafungua simu na kuona biashara ilivyo sasa hivi.
Stawi Biz ni app ya mauzo na ya kutunza kumbukumbu za biashara iliyojengwa kwa biashara za Tanzania: duka, famasi, mgahawa, saluni na lodge. Inapatikana Google Play kwa simu na tablet za Android, na inafanya kazi pia kwenye browser na kwenye kompyuta ya kaunta. Kwenye iPhone, tumia browser; hakuna app ya iPhone kwa sasa.
Duka POS — kuuza, kutunza stock na kuona ripoti ya siku — ni TSh 10,000 kwa mwezi. Vifurushi vyenye daftari la wateja, mauzo ya mkopo na WhatsApp ni TSh 15,000, TSh 25,000 na TSh 35,000. Kila kifurushi kinaanza na siku 14 bure, bila kadi.
Till tu: uza, tunza stock, ona siku
Hakuna daftari la wateja, mauzo ya mkopo wala WhatsApp — hivyo vinaanzia Mwanzo.
Ongeza wateja, mkopo na WhatsApp
Tahadhari, kampeni na hadi matawi matano
Bila kikomo, kupokea mobile money, mafunzo
Google Play, kwa simu na tablet za Android. Tafuta "Stawibiz", au fungua ukurasa wa Pakua kwenye tovuti hii.
Kupakua ni bure na siku 14 za kwanza ni bure bila kadi. Baada ya hapo unachagua kifurushi, kuanzia TSh 10,000 kwa mwezi kwa duka la rejareja.
Ndiyo. App inahifadhi mauzo yaliyofanywa bila mtandao na kuyatuma mtandao ukirudi. Ripoti za mtandaoni na risiti za WhatsApp zinahitaji intaneti.
Hakuna app ya iPhone kwa sasa. Kwenye iPhone, fungua stawibiz.co.tz kwenye browser na uingie kwa akaunti ile ile.
Hapana. Simu inatosha kuanza: kamera yake inasoma barcode. Kompyuta ya kaunta, scanner na printa ya risiti unaweza kuviongeza baadaye.
Mauzo, malipo, stock, matumizi, manunuzi na madeni ya wateja. Kila kimoja kinaingia kwenye ripoti ya siku na kwenye vitabu vya hesabu bila kuandikwa mara ya pili.
Weka bidhaa zako kwenye simu leo, na usome ripoti ya kwanza jioni.