Stawi Biz

Mfumo wa hesabu za biashara unaotunza vitabu kila unapouza.

Kila muuzo, manunuzi, matumizi na malipo yanaingia kwenye ledger ya double-entry papo hapo. Trial balance, faida na hasara na balance sheet viko tayari mhasibu wako anapoviomba — bila mtu kuviandika.

Anza siku 14 bureTuulize kwa WhatsApp
Siku 14 bure. Hakuna kadi.
Leja ya hesabu kwenye simu: mali TSh 320,198,784, balance sheet imelingana, mistari 2,128 ya ledger, na trial balance, faida na hasara na vipindi vinafikiwa kwa mgusa mmoja.

Vitabu halisi, vinavyoandikwa na biashara yenyewe.

Ledger ya double-entry

Chart of accounts kamili: cash, benki, mobile money, wadaiwa, stock, wadai, VAT na mali za kudumu. Kila ingizo linalingana.

Trial balance, faida na hasara, balance sheet

Pamoja na general ledger, cash flow, aging na thamani ya stock. Zipakue kwa PDF, Excel au CSV.

Matumizi yenye idhini

Rekodi matumizi, yapeleke kwa idhini, yalipe. Yanaingia kwenye akaunti sahihi yenyewe.

Ankara na quotation

Quotation, proforma, ankara na credit note zenye letterhead yako. Ankara inaingia kwenye vitabu.

Wadaiwa na taarifa zao

Nani anadaiwa, amechelewa kiasi gani, na taarifa ya kumtumia. Malipo na madeni yaliyofutwa yanarekodiwa.

Mishahara na mali za kudumu

Vipengele vya mshahara, payroll yenye payslip, na mali zenye uchakavu wa kila mwezi.

Anza siku 14 bureTuulize kwa WhatsApp
Siku 14 bure. Hakuna kadi.

Ledger inaandikwa kwenye hatua ileile ya muuzo.

Kwenye biashara nyingi, till na vitabu ni mifumo miwili ambayo mtu huilinganisha mwisho wa mwezi. Hapa muuzo wenyewe ndio ingizo la journal. Vitabu haviwezi kutofautiana na till.

  • Funga kipindi. Funga mwezi uliopita ili takwimu zake zisiendelee kubadilika.
  • Rekebisha, usifute. Ingizo lenye kosa linarudishwa kwa journal, na marekebisho yanabaki kwenye kumbukumbu.
  • Mobile money inalinganishwa. M-Pesa na float nyingine zinalinganishwa na mauzo, na kisicholingana kinaorodheshwa.
Till ya duka: hati ya bidhaa 9 yenye jumla ya TSh 186,500, na kilichobaki stoo kinaonekana chini ya kila bidhaa.

Mfumo wa hesabu za biashara ni nini?

Mfumo wa hesabu ni programu inayorekodi pesa za biashara — mauzo, manunuzi, matumizi, madeni na mali — kama maingizo ya double-entry kwenye ledger, na kuyageuza kuwa taarifa ambazo mmiliki, benki na mhasibu wanazisoma: trial balance, faida na hasara, balance sheet na cash flow.

Stawi Biz ni mfumo wa hesabu uliojengwa ndani ya mfumo wa mauzo kwa biashara za Tanzania. Kwa sababu till, stock na ledger ni mfumo mmoja, vitabu vinaandikwa biashara inapoendelea, kwa shilingi, na mobile money ikiwa na akaunti yake. Muhtasari wa kodi ni ripoti ya ndani; si mawasilisho ya kodi kwa TRA, na Stawi Biz haitoi risiti za EFD wala VFD.

Unamfaa nani?

  • Maduka na wauzaji wa jumla wanaotaka vitabu halisi bila mhasibu wa kudumu.
  • Famasi, migahawa, saluni na lodge — kila moja inaingiza mauzo yake kwenye ledger ileile.
  • Wamiliki wanaoandaa kumbukumbu kwa ajili ya benki, mkopeshaji au mhasibu.
  • Biashara zinazohama kutoka Excel na daftari la cash.

Hesabu ni sehemu ya kifurushi, si nyongeza.

Ledger na taarifa za fedha zinakuja na vifurushi vya aina ya biashara: TSh 15,000, TSh 25,000 na TSh 35,000 kwa mwezi kwa duka la rejareja. Kila kifurushi kinaanza na siku 14 bure, bila kadi.

Duka POS

Till tu: uza, tunza stock, ona siku

TSh 10,000/ mwezi
Watumiaji 2 · Duka 1 · Bila SMS
Anza siku 14 bure
Inajumuisha:
  • Uza kwa simu, kompyuta au till iliyosakinishwa
  • Stock inayopungua kila unapouza, na tahadhari ikikaribia kuisha
  • Mauzo, faida na fedha za leo kwenye simu yako

Hakuna daftari la wateja, mauzo ya mkopo wala WhatsApp — hivyo vinaanzia Mwanzo.

Mwanzo

Ongeza wateja, mkopo na WhatsApp

TSh 15,000/ mwezi
Watumiaji 5 · Duka 1 · SMS 50 bure kwa mwezi
Anza siku 14 bure
Kila kitu cha Duka POS, pamoja na:
  • Daftari la wateja: nani ananunua nini, na mara ngapi
  • Uza kwa mkopo na uone nani anadaiwa
  • Risiti na taarifa kwenye WhatsApp
Inayochaguliwa zaidi

Biashara

Tahadhari, kampeni na hadi matawi matano

TSh 25,000/ mwezi
Watumiaji 15 · Maduka 5 · SMS 200 bure kwa mwezi
Anza siku 14 bure
Kila kitu cha Mwanzo, pamoja na:
  • Ona kila keshia ameuza nini, na saa ngapi
  • Vikumbusho vya madeni vinatoka kwa SMS vyenyewe
  • Tahadhari stock ikipotea, bidhaa ikiacha kuleta faida, mteja wa kawaida akiacha kuja au deni likichelewa
  • Uliza ripoti ya leo kwenye WhatsApp
  • Tuma ofa kwa SMS au WhatsApp kwa wateja wako wote, au kundi lao
  • Ripoti za PDF au Excel, za kupakua, kuchapisha au kutuma
  • Bidhaa, saa na wafanyakazi wanaokuletea faida
  • Wasambazaji, oda za manunuzi na wanachokudai
  • Duka la mtandaoni ambalo wateja wanaagiza

Kampuni

Bila kikomo, kupokea mobile money, mafunzo

TSh 35,000/ mwezi
Wafanyakazi na maduka bila kikomo · SMS 500 bure kwa mwezi
Anza siku 14 bure
Kila kitu cha Biashara, pamoja na:
  • Pokea M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ndani ya app, na link za malipo
  • Msaada wa kipaumbele kwenye WhatsApp
  • Mafunzo kwa wafanyakazi wako
Angalia vifurushi vyote na vilivyomo →

Maswali kuhusu mfumo wa hesabu

Je, Stawi Biz ni mfumo kamili wa hesabu?

Unatunza ledger ya double-entry yenye chart of accounts na kutoa trial balance, general ledger, faida na hasara, balance sheet na cash flow. Vipindi vinaweza kufungwa, na marekebisho yanafanywa kwa kurudisha journal.

Je, lazima niingize mauzo kwenye vitabu mwenyewe?

Hapana. Kila muuzo, manunuzi, matumizi na malipo yanaingia kwenye ledger yanaporekodiwa. Journal za mkono zipo kwa salio la kuanzia na marekebisho.

Je, unawasilisha kodi zangu TRA?

Hapana. Unatoa muhtasari wa kodi kwa kumbukumbu zako na za mhasibu wako. Si mawasilisho ya kodi kwa TRA, na hautoi risiti za EFD wala VFD.

Mhasibu wangu anaweza kuutumia?

Ndiyo. Mpe mhasibu login yake yenye ruhusa unazochagua, naye atasoma ledger na kupakua taarifa.

Naweza kupakua ripoti?

Ndiyo. Ripoti zinapakuliwa kwa PDF, Excel au CSV.

Mfumo wa hesabu unagharimu kiasi gani?

Vifurushi vya rejareja vyenye vitabu kamili ni TSh 15,000, TSh 25,000 na TSh 35,000 kwa mwezi, na siku 14 bure bila kadi.

Acha vitabu vijiandike kwa siku 14.

Uza kama kawaida kwa wiki mbili, kisha fungua trial balance.

Anza siku 14 bureTuulize kwa WhatsApp