Skani au andika, pokea cash, M-Pesa au mkopo, na risiti iko kwenye WhatsApp ya mteja kabla hajaondoka. Stock, madeni na ripoti ya siku yako vinabadilika kila muuzo — kwa simu, kompyuta, au till iliyosakinishwa inayoendelea kuuza mtandao ukikatika.
Kamera ya simu yoyote inafanya kazi kama scanner, au chomeka scanner halisi. Andika herufi tatu na bidhaa inatokea.
Cash na chenji, M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, HaloPesa, benki, au mchanganyiko. Au weka kwenye akaunti ya mteja.
Au inachapishwa kwenye printa ya risiti kama unayo. Vyovyote, mteja anayo kabla hajafika mlangoni.
Kila bidhaa inaonyesha kilichobaki, na inakuonya kabla haijaisha. Uza kwa kipande, dazeni au katoni.
Fungua zamu, ifunge, na uone fedha iliyotarajiwa dhidi ya iliyohesabiwa. Droo pungufu inaonekana jioni hiyohiyo.
Kurudisha pesa au muuzo uliofutwa unarekodiwa, na nani alifanya na kwa nini. Hakuna kinachopotea kimyakimya.
Mtandao unakatika. Kaunta haiwezi. Desktop POS inasakinishwa kwenye kompyuta ya duka na inauza bila intaneti kabisa; mauzo ya simu yanapanga foleni na kusawazishwa mtandao ukirudi.

Mfumo wa mauzo (POS) ni programu inayorekodi kila muuzo unapofanyika — bidhaa, bei, njia ya malipo na mteja — na kusasisha stock, madeni na ripoti papo hapo. Badala ya daftari na kalamu, kila muamala unaingia kwenye mfumo mmoja unaoonekana kwenye simu, kompyuta au desktop POS iliyosakinishwa.
Stawi Biz ni mfumo wa mauzo uliojengwa kwa biashara za Tanzania: duka la rejareja, famasi, mgahawa na saluni. Unarekodi mauzo ya cash, mobile money na mkopo, unatuma risiti kwa WhatsApp, unafuatilia stock kwa barcode, na unampa mmiliki ripoti ya siku bila kusubiri kufunga. Uuzaji offline umewekewa mipaka kwenye desktop POS iliyosakinishwa na foleni ya mauzo ya simu; ripoti za mtandaoni zinahitaji intaneti.
Duka POS — kuuza, kutunza stock na kuona ripoti ya siku — ni TSh 10,000 kwa mwezi. Vifurushi vya rejareja vyenye daftari la wateja, mauzo ya mkopo, WhatsApp na zaidi ni TSh 15,000, TSh 25,000 na TSh 35,000. Kila kifurushi kinaanza na siku 14 bure, bila kadi.
Till tu: uza, tunza stock, ona siku
Hakuna daftari la wateja, mauzo ya mkopo wala WhatsApp — hivyo vinaanzia Mwanzo.
Ongeza wateja, mkopo na WhatsApp
Tahadhari, kampeni na hadi matawi matano
Bila kikomo, kupokea mobile money, mafunzo
Ni programu ya kurekodi mauzo, malipo na stock kwa wakati mmoja. Kila muuzo unapoingizwa, stock inapungua, deni la mteja linasasishwa na ripoti ya mmiliki inabadilika papo hapo.
Desktop POS iliyosakinishwa inaendelea kuuza mtandao ukikatika, na foleni ya mauzo ya simu inahifadhi mauzo hadi intaneti irudi. Dashibodi, ripoti za mtandaoni na risiti za WhatsApp zinahitaji intaneti.
Ndiyo. Famasi inaendeshwa kama aina yake ya biashara, yenye ufuatiliaji wa batch, tahadhari za expiry na kumbukumbu za madai. Duka lenye kaunta ya famasi linaongeza aina ya pili kwa nusu bei yake.
Ndiyo — siku 14 bure kwenye kifurushi chochote, bila kadi.
Ndiyo. Risiti zinaenda kwa mteja kwenye WhatsApp anapolipa, na ripoti za siku zinaweza kutumwa kwa mmiliki pale njia ya WhatsApp imesanidiwa.
Kwenye simu, kivinjari cha kompyuta, na desktop POS iliyosakinishwa. Scanner za barcode na printa za risiti zinazoungwa mkono zinaunganishwa moja kwa moja.
Leta bidhaa zako, uza kwa wiki mbili, na uone kama ripoti ya jioni inakuambia kitu kipya.