Stawi Biz

POS ni nini?

POS ni kifupi cha point of sale, yaani mahali na wakati mteja anapokulipa. Mfumo wa POS ni programu, na wakati mwingine kifaa cha kaunta, kinachorekodi mauzo hayo na kusasisha kila kitu kinachohusika.

Anza siku 14 bureTuulize kwa WhatsApp

Mfumo wa POS unafanya nini

Mteja akinunua, mfumo wa POS unafanya kwa sekunde chache kile daftari linachofanya kwa jioni nzima.

  • Unarekodi mauzo: nini kimeuzwa, kwa bei gani, punguzo lipi, na nani amelipa.
  • Unapokea malipo, ya pesa taslimu, ya simu (M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa) au kadi.
  • Unampa mteja risiti, ya karatasi au ya WhatsApp.
  • Unatoa bidhaa kwenye stoo wenyewe, ili orodha ya stoo iwe sahihi ukifungua kesho.
  • Unatunza deni mteja akilipa baadaye, jina likiwa pembeni yake.

Kwa nini daftari au Excel havitoshi tena

Daftari linatosha ukiwa wewe peke yako unauza na unakumbuka kila kitu. Halitoshi tena wafanyakazi wakiuza ukiwa mbali, wateja wakichukua bidhaa kwa mkopo, au ukipokea pesa taslimu na pesa za simu kisha jumla za usiku hazilingani.

Tatizo mara nyingi si mauzo uliyoandika. Ni yale ambayo hakuna aliyeandika, bidhaa zilizotoka bila kumbukumbu, na madeni ambayo hakuna anayekumbuka.

Dalili kwamba duka lako linauhitaji

  • Huwezi kusema bila kuhesabu kilichobaki kwenye rafu.
  • Wafanyakazi wanauza ukiwa hupo, na unakuja kujua baadaye.
  • Wateja wanachukua bidhaa kwa mkopo na huna uhakika nani anadaiwa nini.
  • Pesa taslimu na pesa za simu hazilingani mwisho wa siku.
  • Unataka kujua faida yako, si mauzo tu.

Cha kuangalia kabla ya kuchagua

  • Unaendelea kuuza mtandao ukikatika na kujiunganisha baadaye.
  • Stoo na madeni viko pamoja na mauzo, si kwenye zana nyingine.
  • Kila mfanyakazi ana ufikiaji wake, si nenosiri moja la kila mtu.
  • Unafanya kazi kwa Kiswahili, na kwenye simu au kompyuta uliyonayo.
  • Unaweza kujaribu kabla ya kulipa, ukitumia bidhaa zako mwenyewe.

Stawi Biz inaingia wapi

Stawi Biz ni mfumo wa POS na wa biashara kwa maduka, famasi, migahawa, saluni, klabu na hoteli za Tanzania. Kaunta inauza hata mtandao ukikatika, inapokea pesa taslimu na pesa za simu, inatuma risiti kwa WhatsApp, na inatunza stoo na madeni ya wateja mahali pamoja. Unaweza kujaribu bure kwa siku 14.

POS ni sawa na mashine ya kuhesabia pesa (cash register)?

Cash register inarekodi pesa zinazoingia tu. Mfumo wa POS pia unafuatilia stoo, madeni ya wateja, wafanyakazi na ripoti, kwa hiyo unaona biashara nzima, si kaunta peke yake.

Je, POS inafanya kazi bila intaneti?

Nyingine zinafanya. Kaunta ya Stawi Biz inaendelea kuuza mtandao ukikatika, na inatuma mauzo yakirudi mtandaoni.

Nahitaji vifaa maalum?

Hapana. Simu, tablet au kompyuta inatosha kuanza. Scanner ya barcode au printer ya risiti inasaidia, ila unaweza kuongeza baadaye.

POS inagharimu kiasi gani Tanzania?

Inategemea kifurushi na aina ya biashara. Ukurasa wa bei unaonyesha kila kifurushi, na kuna jaribio la siku 14 bure ili ujaribu kabla ya kulipa.

Bei ya mfumo wa POS na mambo sita ya kuangaliaPOS ya Stawi Biz kwa madukaDuka linahitaji nini kwenye mfumo

Ujaribu na bidhaa zako.

Weka duka lako kwa dakika chache na uuze nalo siku 14 bure, bila kadi.

Anza siku 14 bureTuulize kwa WhatsApp